Kuelekea michuano ya kombe la Dunia ambayo mwaka huu inatarajiwa kufanyika nchini Urusi kuanzia June 14, katika kipindi cha Zaidi kimeweza kufanya tafiti mbalimbali juu ya makombe ya dunia yaliyowahi kufanyika miaka ya nyuma.
Katika tafiti hizo kuna rekodi mbalimbali zilizovunjwa na baadhi ya nchi ambapo kuna nchi zimeweza kuchukua kombe hilo zaidi ya mara tano.
Aidha mara nyingi imekuwa ikitokea nchi inayokuwa wenyeji wa michuano ya kombe la dunia huwa na asilimia kubwa ya kuchukua kombe hilo, Je mwaka huu Urusi itatwaa kombe hilo?.
Bonyeza kitufe chekundu kutazama rekodi mbalimbali za nchi zilizowahi kuchukua kombe la dunia mara nyingi zaidi.