Wakili wa kujitegemea, Leonard Manyama amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuwabana viongozi ili kuwaweka mbali na mgongano wa kimaslahi.
Ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Dar24Media, ambapo amesema kuwa kiongozi mwenye mgongano wa maslahi hawezi kutenda haki.
Amesema kuwa bara la Afrika limepita katika wakati mgumu wa uvunjaji wa haki za binadamu, hivyo nchi nyingi zimepiga hatua katika kutetea haki.
“Kwakweli hatuwezi kulinganisha tulikotoka, kwasasa tumeiga hatua, ambapo watu wanaheshimu haki za binadamu, kuna uhuru na demokrasia,”amesema Wakili Manyama