Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imepanga kujenga barabara mbili kuu za lami ambazo zikikamilika zitasaidia kuunganisha mikoa mitano ya Arusha, Singida, Simiyu, Shinyanga na Manyara.

Majaliwa amesema hayo kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Haydom na Mbulu Mjini kwenye mikutano wa hadhara iliyofanyika wilayani Mbulu, mkoani Manyara.

Amezitaja barabara hizo kuwa ni ya kutoka Karatu-Mbulu- Haydom-Sibiti- Lalago- Meatu hadi Maswa yenye urefu wa km. 389 (maarufu kama Serengeti Southern Bypass) na nyingine ni ya kutoka Haydom hadi Katesh yenye urefu wa km. 74. Pia limo daraja la Magara linalounganisha Mbulu na Babati.

“Fedha kwa ajili ya upembuzi wa awali imeshatolewa na kazi imeshaanza kwa ajili ya barabara ya kutoka Karatu-Mbulu- Haydom-Sibiti- Lalago hadi Meatu na Maswa lakini hii ya Katesh hadi Haydom itaombewa fedha kwenye bajeti tunayoiandaa hivi sasa.”

 

Video: Maamuzi ya Mahakama kuhusu Mbowe
Keylor Navas Awa Kivutio SS Napoli