Serikali ya Tanzania imekanusha vikali tuhuma ambazo zimekuwa zikitolewa wa baadhi ya wanasiasa nchini Kenya kuwa tayari imeshaweka mitambo Kigamboni Jijini Dar es salaam kwaajiri ya kuchakachua matokeo ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo unaotarajiwa kufanyika Agosti 8 mwaka huu.
Hayo yamesemwa Jijini Dar es salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Augustine Mahiga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, amesema kuwa taarifa hizo ni za uzushi na wala hazina ukweli wowote kwani Tanzania na Kenya ni nchi marafiki.
Amesema kuwa tuhuma hizo zinazoenezwa na vyombo vya habari na baadhi ya vyama vya upinzani nchini Kenya na hapa Tanzania siyo za kweli na ametoa tahadhali kwa wale wote watakaobainika kujihusisha na uchakachuaji huo watachukuliwa hatua kali.
“Lakini nachukua nafasi hii kutoa taarifa kwa mara nyingine tena, hakuna mtu anayetakiwa kuwa wasiwasi wowote, siasa ya Tanzania haitaingilia siasa za Kenya, ifahamike hivyo suala la uchaguzi na kuhesabu kura ni la Wakenya wenyewe,”amesema Mahiga.
- JPM: Nitachomoa mwingine mwenye akili kutoka upinzani
-
Majaliwa awatega wakuu wa mikoa ya Mbeya na Songwe
-
Video: Tanzania na Kenya zamaliza tofauti zao za kibiashara
Hata hivyo, siku za hivi karibuni kumekuwepo na taarifa ambazo zimekuwa zikienezwa na baadhi ya wanasiasa wa upinzani nchini Kenya na Tanzania kwenye vyombo vya habari kuhusu Tanzania kuingilia uchaguzi mkuu nchini Kenya.