Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Kenya zimefanya mazungumzo ya pamoja na kutatua vikwazo vilivyokuwa vikiikabili sekta ya biashara baina ya nchi hizo.

Hayo yamesemwa na mapema hii leo Jijini Dar es salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo ametoa taarifa juu ya kumalizika kwa tofauti za kibiashara baina ya nchi hizo.

“Bidhaa za Tanzania zilizowekewa vikwazo na nchi ya Kenya ni unga wa ngano pamoja na  gesi ya kupikia (LPG) juhudi za Serikali ya Tanzania kuona vikwazo hivyo vinaondolewa na Serikali ya Kenya kwa wakati hazikuzaa matunda, hivyo Serikali ya Tanzania nayo iliweka vikwazo kwa bidhaa za maziwa na sigara kutoka Kenya kuingia katika soko la Tanzania,” amesema Dkt. Mahiga.

Amesema kuwa kutokana na mahusiano mazuri ya udugu yaliyopo kati ya Tanzania na Kenya na  kwa kujali manufaa mapana ya Jumuiya ya Afrika Mashariki viongozi wakuu wa nchi hizo mbili, Rais wa Jamhuri ya Kenya, Uhuru Kenyatta na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli walikubaliana kuzungumza na kutoa vikwazo vya biashara hizo.

 

Video: Chama cha ADC chamuomba JPM kulegeza masharti ya siasa
Majaliwa awatega wakuu wa mikoa ya Mbeya na Songwe