Serikali imeokoa zaidi ya shilingi milioni 600 ambazo zingetumika kuwasafirisha wagonjwa 15 kwenda nje kutibiwa mfumo wa umeme wa moyo na sasa wagonjwa hao wanapata huduma hiyo hapa hapa nchini.
Aidha, wagonjwa hao wanapatiwa huduma hiyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika kambi maalum ambapo madaktari kutoka Marekani watashirikiana na madaktari wa Taasisi hiyo.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Tiba ya Moyo wa taasisi hiyo, Peter Kisenge ambapo amesema kuwa wagonjwa watakaopatiwa huduma hiyo ya upasuaji ni wale ambao mioyo yao imechoka na wale ambao mapigo yao ya moyo yako chini watawekewa betri maalum.