Serikali imetangaza mfumo mpya wa usajili na utoaji wa leseni za uchapishaji wa magazeti ili kuweza kufikia malengo iliyojiwekea ya muendelezo wa kuifanya Tasnia hiyo kuwa Taaluma ya Habari.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa lengo la kuweka mfumo huo ni kuiweka tasnia ya habari kuwa taaluma kamili kama zilivyo zingine.
“Mfumo huu ambao Serikali imeuweka una lengo moja tu la kuisadia tasnia ya habari kuwa taaluma ili kuwepo uwajibikaji kwa kila mmoja kwenye chombo chake anachofanyia kazi na serikali kwa ujumla,”amesema Dkt. Abbas
Hata hivyo, Serikali imesema kuwa kuanzia leo magazeti yote yanatakiwa kusajiliwa upya kwa mfumo huo wa leseni, hivyo mwisho wa usajili huo ni Oktoba 11 mwaka huu.