Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) Julius Mtatiro amebainisha sababu zilizomng’oa ndani ya chama hicho na kuomba kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo amesema kuwa amefanya hivyo ili kufanya siasa za maendeleo ili kumsaidia Rais Dkt. Magufuli

Mtatiro ametangaza kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa ameanza kwa kuzungumza na waandishi na kutangaza azma yake ambayo ameitafakari kwa muda mrefu kabla ya kuwataarifu viongozi wa CCM ambao amewaomba wampokee.

“Nawaambia Watanzania kwamba kuanzia leo nitaanza kufanya siasa za maendeleo ili kumsaidia Rais John Pombe Magufuli,”amesema Mtatiro

 

Zitto: Wajibu wangu kuiharibu CCM, mtasubiri sana
Ridhiwani Kikwete awaasa wazazi kusomesha watoto masomo ya Sayansi