Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amesema kuwa hatafuta Mwenge wa Uhuru katika kipindi chake cha uongozi kwasababu una faida mbalimbali kwa taifa.
Ameyasema hayo mapema hii leo kwenye hotuba yake wakati akihitimisha mbio za Mwenge mwaka huu sambamba na kuazimisha miaka 18 ya kifo cha Baba wa Taifa kwenye sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Amani Zanzibar.
Aidha, Rais Magufuli amesema kuwa awamu yake kamwe hatafuta mbio hizo kwani zina saidia kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo nchini pamoja na kumuenzi Baba wa taifa Hayati Mwalimu Nyerere ambaye ndiye muasisi wa Mwenge wa Uhuru.
“Nafahamu kuna watu wanataka mbio za Mwenge zifutwe kwa kisingizio cha gharama lakini wanasahau kuwa Mwenge huo unasaidia kuanzishwa na kukamilika kwa Miradi ya maendeleo nchini. Nataka niwahakikishie kuwa kwenye uongozi wangu na Dkt. Shein hatutafuta Mwenge wa Uhuru”, amesema Rais Magufuli
-
Video: Prof. Mwandosya atema nyongo, Sharti la uchaguzi lazua hofu CCM
-
Ponda aendelea kushikiliwa na Polisi
-
Magufuli aahidi kuuenzi Mwenge
Hata hivyo, ameongeza kuwa mbio za Mwenge zimekuwa zikisaidia kubaini madudu mbalimbali yanayofanyika kwenye Halmashauri nchini ikiwemo Miradi hewa. Rais ameahidi kuipitia ripoti nzima ya mbio hizo na kuyafanyia kazi mapendekezo yote yaliyoainisha