Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezindua kampeni inayosema Usinitumie, Sitaki, Situmii wengine, nitakuripoti kwa lengo la kudhibiti na kusisitiza matumizi salama na sahihi ya mitandao ya kijamii.
Hayo yamezungumzwa jana na Mwenyekiti wa Bodi ya TCRA, Jones Kilembe ambapo amebainishwa kuwa kutokana na ukuaji wa teknolojia ya mawasiliano, matumizi ya mitandao yameongezeka jambo ambalo limevutia wasio na taaluma ya habari na wale wenye taaluma kuleta changamoto kadhaa, ikiwa ni pamoja na kutofuata maadili.
-
Video: Mbowe apinga kuondolewa kwa Lissu Kenya, anena mazito
-
Serikali kuchochea maendeleo kupitia mawasiliano
” kwa sasa tuna zaidi ya televisheni za mtandaoni 50, zaidi ya blogu 150 na maendeleo ya teknolojia na kuanza matumizi ya simu za kisasa imechangia udhibiti wa maudhui kuwa mgumu, jambo ambalo imeifanya TCRA kusisitiza ufuatiliaji wa karibu kwa maendeleo ya nchi kijamii, kiuchumi na siasa,” amesema Dk Jones.
-
LIVE: Rais Magufuli akiwatunuku kamisheni wanafunzi JWTZ
-
Prof. Mbarawa anena kuhusu baraza la ujenzi NCC
Jeshi la polisi limebainisha kuwa uhalifu wa mtandao unaoongoza hasa katika utumiaji na usambazaji wa taarifa za uongo, takwimu zimeonesha kuwa kesi zilizoripotiwa polisi kwa 2015 makosa ya mtandaoni ni 5,172 huku kwa mwaka 2017 namba ya makosa ya kimtandao ilishuka kwa kiwango kidogo ambapo takwimu zinaonesha kuwa makosa yaliyoripotiwa ni 3346.
TCRA imesema lengo kubwa la kampeni hiyo ni kutoa elimu kwa umma na matumizi salama na sahihi ya mitandao na kwamba kwa kufanya hivyo uhalifu wa mitandaoni utapungua kwa asilimia 90.
Tazama video inayohamisisha kampeni hiyo ya kudhibiti mitandao ya kijamii.