Idara ya Uhamiaji imesema kuwa Hati mpya za kusafiria za ‘Kielectronic’ zitakuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi ambao wamekuwa wakipata usumbufu mkubwa.

Hayo yamesemwa hii leo Jijini Dar es salaam na Msemaji wa Idara ya Uhamiaji, Ali Mtanda alipokuwa akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema kuwa hati hizo za kusafiria zitamrahisishia mtumiaji wa hati hiyo kuondokana na usumbufu pindi inapokuwa imepotea.

Amesema kuwa hati hizo zina manufaa makubwa kwani mtumiaji anaweza kuipata popote alipo na kuweza kuhakikiwa taarifa zake.

“Hii imewekwa kwa lengo la kuwasaidia Watanzania kuondokana na usumbufu pindi wanapokuwa wamepotelewa na hati zao za kusafiria hasa wanapokuwa wako nje ya nchi,”amesema Mtanda

 

Majibu ya Serikali matumzi ya sindano za kuongeza maumbile
Prof. Kamuzora afanya ukaguzi kituo cha Mawasiliano ya dharura