Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa Serikali haijazuia wanafunzi wa kike kuendelea na masomo baada ya kupata ujauzito bali ilizuia mwanafunzi kurudi shule aliyokuwa akisoma awali.

Ameyasema hayo hii leo Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali ambalo liliulizwa na Mbunge wa Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CHADEMA, Halima Mdee.

“Ni kweli kulikuwa na maandalizi ya ‘re entry policy’ lakini utekelezaji wake sasa umepitwa na wakati kutokana na agizo lililotolewa na Serikali kwamba mtoto ambaye amepata ujauzito hataruhusiwa kurudi katika shule ambayo alikuwa anasoma lakini maagizo haya hayajazuia mtoto wa kike ambaye amepata ujauzito kutoendelea na masomo hapo naomba tuelewane vizuri,”amesema Dkt. Ndugulile

Amesema kuwa sasa Serikali inaangalia njia mbadala ambayo itawawezesha watoto wa kike ambao wamepata ujauzito kuendelea na masomo.

Kwa upande wake Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa. Joyce Ndalichako amesema kuwa  msimamo wa Serikali kuwa mwanafunzi ambaye amepata ujauzito hawezi kurudi shule.

 

Mahakama kuingia katika mfumo wa kielektroniki
Peneza: Elimu bure iende sambamba na utoaji bure wa Pedi kwa wasichana