Serikali imetangaza ununuzi wa korosho wa msimu mpya unaohusisha teknolojia ya wanunuzi kujisajili kwenye Bodi ya Korosho kupitia mfumo wa Wizara ya Kilimo wa kusimamia Biashara za Kilimo (Agricultural Trade Management Informataion System – ATMIS).
Imeeleza pia kuhusu deni la korosho msimu uliopita inalodaiwa na wakulima wakubwa kuwa shilingi bilioni 50, ambalo linaendelea kulipwa kila siku kulingana na shehena ya korosho zinazonunuliwa na wanunuzi.