Mbunge wa Mbeya Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joseph Mbilinyi amesema kuwa Idara ya Magereza haithaminiki kiasi cha kutotengewa bajeti ya kutosha.
Ameyasema hayo Jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na Dar24 Media, ambapo amesema kuwa Gereza alilokuwa amefungwa kisiasa la Luanda lililopo Jijini Mbeya lina uwezo wa kuchukua wafungwa 400 lakini mpaka sasa lina wafungwa 1400.
Amesema kuwa changamoto kubwa inayoikabiri Idara hiyo ni ukosefu wa fedha ambao unapelekea mlundikano mkubwa wa wafungwa katika Magereza.
“Hii yote inatokana na watu kubambikizwa kesi huku wakijua kuwa hakuna nafasi ya kutosha na Magereza yana uwezo mdogo wa kuchukua wafungwa,”amesema Sugu
-
Video: Azuiliwa hospitalini kwa miezi 5 kwa kushindwa kulipa deni la milioni 8
-
Video: Huu ni ukatili, huwezi kumuua mwenzio kwa wivu wa mapenzi- Dkt. Bisimba
-
Tril 1.5 zataka kumng’oa Waziri, Ndugai amwokoa Mwenyekiti sekeseke la wapinzani bungeni