Katika eneo lenye mzozo la Tigray nchini Ethiopia, kiwango cha vifo vya watoto wanaokufa katika mwezi wao wa kwanza wa maisha ni mara nne ya kiwango cha kabla ya vita, ikiwa ni taarifa iliyotokana na utafiti wa hivi karibuni.

Taarifa hiyo inasema, sababu za kawaida zilikuwa kabla ya wakati, maambukizo na ukosefu wa hewa wakati wa kuzaa, au kutokuwa na uwezo wa kuanza kwa upumuaji wakati wa kuzaliwa hali ambayo ni chanzo cha vifo vya watoto chini ya miaka mitano.

Hata hivyo, wakati wa vita vifo hivyo viliongezeka maradufu ikilinganishwa na enzi ya kabla ya vita huku ikimaanisha kuwa vifo vya watoto katika vitengo kwa siku 28 za kwanza za maisha, viliongezeka mara nne, ikilinganishwa na enzi za kabla ya vita kutoka karibu 10.

Tafiti hiyo iliyofanyika huko Tigray mwaka 2020, inasema hadi karibu 36, huku Daktari wa watoto katika Hospitali ya Rufaa ya Ayder, Dk. Bereket Berhe akisema takriban miaka miwili imepita tangu vita kuanza na serikali ya Ethiopia ilitenga eneo la Tigray na kukata huduma za msingi kama vile umeme, simu, mtandao na benki.

Pande zote mbili zimealikwa katika mazungumzo ya amani ya Umoja wa Afrika mwishoni mwa juma hili nchini Afrika Kusini na licha ya Serikali kuthibitisha ushiriki wake, upandewa waasi haujasema kitu lakini inahisiwa watakuwepo katika mkutano huo ili kuweza kutafuta amani ya kudumu ya Tigray.

Wazazi 'wanena' wito wa Polisi wahitimu Darasa la saba
Wizara ya Afya yathibitisha uwepo homa ya Nguruwe