Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno amesema Jeshi hilo linawashikilia watu wawili kwa mahojiano huku msako ukiendelea kufanyika kwa tuhuma za mauaji ya mwanafunzi wa shule ya msingi Mtumba, Farida Makuya (16) ambaye  aliuawa usiku wa Oktoba 4, 2022 nyumbani kwao Mtumba Dodoma.

Otieno amesema, “Kwa sasa tumewakamata watu wawili kwa mahojiano, tunaendelea na msako mkali, kwa kitendo hiki lazima wahusika wakamatwe na watiwe mbaroni, lakini hili ni tukio baya, baya, baya sana lazima tushughulike nao,” amesema Otieno.”

Farida alitakiwa kufanya mitihani ya kumaliza elimu ya msingi iliyoanza jana na kutarajiwa kumalizika leo Alhamisi ambapo mwili wake ulizikwa jana katika makaburi ya Mtumba na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa jiji la Dodoma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno.

Oktoba 5, 2022 Mjomba wa marehemu, Anderson Makuya akizungumza alisema usiku wa Oktoba 4, 2022, alipokea simu kutoka kwa ndugu zake kwamba mjomba wake amepigwa na watu wasiojulika na amepelelekwa hospitali ya Rufaa ya Dodoma kwa ajili ya kupatiwa  matibabu.

Amesema, “Mjomba wangu alipaswa kufanya mitihani yake ya darasa la sabana siku ya tukio mama wa marehemu alienda kuuza pombe za kienyeji hapa hapa Mtumba na aliiondoka nyumbani kwake bila kurudishia mlango ili akirudi iwe rahisi kuingia ndani, alirudi majira saa nane usiku na aliingia moja kwa moja ndani kwani mlango ulikuwa haujafungwa.”

“Baadaye aliona michirizi ya damu baada ya kuwasha tochi ya simu, alishtuka na kuifuata michirizi hiyo mpaka nyuma ya nyumba karibu na uwanja wa mpira akakuta marehemu akiwa ametupwa hapo huku damu nyingi zikitoka kichwani, wakamchukua na kumpeleka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na kabla hawajafika alifariki.” Alisimulia mjomba wa Marehemu Makuya.

Dawa za maji kusababisha kansa
'Panya road' 40 wafikishwa Mahakamani