Watu 40, akiwemo Lubea Manzi ambaye ni maarufu kwa jina la ‘Master’ hii leo Oktoba 6, 2022 wamefikishwa mbele ya Mahakimu watatu wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala Mkoani Dar es Salaam, kusomewa mashtaka ya unyang’anyi wa kutumia silaha, kuvunja nyumba usiku na kujeruhi watu maeneo mbalimbali.

Waendesha mashtaka mawakili wa serikali, Michael Momboko, Magdalena Kisoka, Aziza Mhina mbele ya Mahakama walisema kuwa watuhumiwa hao walitenda makosa hayo kati ya tarehe 19 – 21/09/ 2022 katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam.

Washtakiwa wakiwa chini ya Ulinzi katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam hii leo Oktoba 6, 2022.

Wamesema, washtakiwa hao walivunja nyumba usiku na walipora mali baada ya kuwajeruhi wananchi kwa kutumia silaha za jadi (mapanga, nondo, visu) na kukimbia.

Hata hivyo, wakiwa mbele ya Hakimu Mkazi Glory Nkwera, Fadhili Luvinga, Rehema Liana, Watuhumiwa hao kwa pamoja walikana mashtaka na kurudishwa rumande kutokana na mashataka wanayowakabiliwa nayo kutokuwa na dhamana huku kesi hiyo ikiharishwa mpaka hadi Oktoba 19, 2022 na upelelezi wa shauri hilo umekamilika.

Mauaji Mwanafunzi Darasa la Saba: Wawili washikiliwa na Polisi
TRA yaonya 'Plate Number' zisizo rasmi