Mwenyekiti wa Chama cha ACT -Wazalendo Taifa, ndugu Juma Duni Haji, amesema vijana wengi kwasasa hawana maadili na hivyo wamekosa mwelekeo na kuhimiza wananchi kuunganisha nguvu kwa pamoja ili kuwasaidia kuwa na dira njema ya kuchangia ujenzi wao kimaisha na Taifa kiujumla.

Juma Duni ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika Bumbwini Makoba, wa kukamilisha mzunguko wa kwanza wa mikutano ya aina hiyo tangu kuruhusiwa kwa mikutano ya kisiasa, miezi michache iliyopita.

Katika mkutano huo, Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Zanzibar, Othman Masoud Othman pia alisema Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, ni ngome ya Wazanzibari na kwamba Serikali inawajibu wa kusimamia masuala yanayoamuliwa na kusimamiwa na chombo hicho, kwa niaba ya wananchi.

Naye Mwenyekiti wa Ngome ya Wanawake wa Chama hicho Taifa, Pavu Abdalla Jumameitaka serikali kukaa pamoja na wananchi wa kijiji hicho kutafuta namna bora ya kuondoa manung’uniko ya suala hilo ikiwa ni pamoja na kutumia utaratibu wa wananchi kukodisha ardhi zao ili wanufaike zaidi kuliko ilivyo sasa.

FC Bayern Munich yachora mstari
Nipo tayari kufa, Jela mateso - Mchungaji Mackenzie