Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira Anthony Mavunde, amesema asilimia kubwa ya Vijana nchini wamejiajiri katika sekta ya Kilimo, baada ya kuondokana na dhana ya kuajiriwa.

Mavunde ameyasema hayo hii leo jijini Dodoma, katika hafla ya kuwakabidhi pikipiki za biashara Vijana 30 kutoka mikoa mitano nchini, iliyoratibiwa na kampuni ya Route Pro.

Amesema vijana wengi wameathiriwa na dhana ya kuajiriwa katika sekta binafsi, mashirika mbalimbali na Serikali, kitu ambacho huwachelewesha kufikia malengo na ndoto walizojiwekea maishani.

“Ukosefu wa ajira kwa vijana imekuwa ni changamoto kwa Taifa letu, na ili kukabiliana na hili Serikali imekuwa ikitoa kipaumbele kwa kushirikiana na wadau kubuni mipango endelevu ya ya uwezeshaji ajira.” amesema Naibu Waziri Mavunde.

Awali akizungumza katika hafla hiyo, Meneja uratibu wa Kampuni ya Route Pro Jaja Mbazila, amesema wamelenga kuwawezesha vijana wenye bidii ya kazi na kujituma ili kukuza mitaji yao.

Amesema mbali na kuwapatia pikipiki hizo, pia vijana hao watapata kiasi cha shilingi laki moja kila mmoja, kitakacho wawezasha kuanzia kazi kama moja ya hamasa itakayowafanya kupambana kibiashara.

“Zipo fursa nyingi lakini ni vyema kuzitumia ipasavyo ili vijana waweze kujiinua kimaisha, maana wengi wa vijana huwa wanaonesha nia ya kufanya vizuri na nina imani wanaweza.” Amefafanua Mbazila.

Vijana hao 30 kutoka mikoa ya Dodoma, Dar es Salaam, Singida, Moshi na Arusha, mbali na kupatiwa pikipiki hizo pia wamejifunza njia mbalimbali za kufanikiwa kupitia biashara ya usambazaji.

  • Error: Contact form not found.

 

Changamoto za sekta ya Afya nchini kupatiwa ufumbuzi
Mshtakiwa aomba kujidhamini adai sehemu zake za siri zimetoweka