Mkutano wa kwanza wa kilele kuhusu Tabianchi Barani Afrika, umeanza hii leo jijini Nairobi, Kenya ambapo takriban Viongozi 20 wa nchi na Serikali wa Afrika na wajumbe 20,000 kutoka Duniani kote wanakutana, ili kujadiliana kimtazamo na kuwasilisha hoja zao katika mkutano mwingine uliopangwa kufanyika Desemba 2023 huko Dubai.
Hata hivyo, washiriki wanataka vitendo wakisema hakuna haja ya kukutana bila matokeo yoyote chanya, kama inavyokuwa mara nyingi wakati wa mikutano kama hiyo, huku Rais wa Kenya, William Ruto ambaye ni mwenyeji wa hafla hiyo, akitaka mkutano huu ulete mabadiliko ya kimazingira.
Iwapo jambo hili litatimia, itakuwa ni dhamira dhabiti barani Afrika, chini ya miezi mitatu kabla ya COP28, ambayo inaanza mwishoni mwa Novemba huko Dubai na Nchi za bara la Afrika ni miongoni mwa nchi zilizo hatarini zaidi na mabadiliko ya tabianchi, zikikabiliwa na ukame, mafuriko, vimbunga namajanga ya asili yanaongezeka.
Hata hivyo, hitaji la usanifu mpya wa kifedha kwa ajili ya hali ya hewa kwa hivyo linapaswa kuwa kiini cha majadiliano, karibu na urekebishaji wa madeni, ikiwemo uanzishaji wa ushuru kwenye mafuta ya kisukuku na tasnia zinazochafua mazingira, kama vile usafiri wa anga na baharini.