Ujumbe wa wakuu wa nchi za Afrika, wamekutana na Viongozi wa Serikali ya Ukraine ikiwa ni sehemu ya juhudi za upatanishi na matumaini ya kuanzisha kwa mazungumzo ya amani, kati ya Ukraine na Russia.
Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa ni miongoni mwa ujumbe huo wa Umoja wa Afrika, ambao unakutana na Rais wa Ukraine, Volodymr Zelenskiy ili kutafuta makubaliano ya amani kati ya Kyiv na Moscow.
Wajumbe wengine walio katika msafara huo ni Rais wa Senegal, Macky Sall, Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema na Rais wa Comoro, Azali Assoumani ambaye ni Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika.
Marais wengine watatu, wa Jamhuri ya Congo, Misri na Uganda walitarajiwa kushiriki katika msafara huo lakini kutokana na sababu mbalimbali walituma wawakilishi, na wote kwa pamoja pia wataelekea Russia kukutana na Rais Vladimir Putin.