Hali ya usalama, imezidi kuimarishwa jijini Mogadishu, Viongozi wa kikanda wakikutana hii leo (Februari 1, 2023), nchini Somalia, kujadili mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la Al Shabab.

Viongozi hao, kutoka nchini Kenya, Ethiopia na Djibouti walitarajiwa kuhudhuria mkutano huo unaokuja wakati huu jeshi la Umoja wa Afrika ATMIS, lilikishirikiana na lile la Somalia na makundi yenye silaha yanayoungwa mkono na serikali, kufanikiwa kudhibiti baadhi ya miji kutoka kwa Al Shabab.

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud. Picha ya RFI.

Umoja wa Afrika ambao una wanajeshi 20,000, unalenga kumalizika kwa operesheni zake kufikia mwishoni mwa mwaka 2024 na kuacha jukumu la usalama kwa jeshi la serikali.

Tangu alipochukua madaraka mwezi Mei mwaka uliopita, Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud, alitangaza vita dhidi ya Al Shabab, kundi ambalo limeendelea kuwa hatari kwa usalama wa nchi hiyo na ukanda wa pembe ya Afrika.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Februari 2, 2023
Ashikiliwa kwa kumuuwa mkewe na kumzika kisimani