Maafisa wakuu wa Taliban wametoa wito wa msaada wa kimataifa ili kukabiliana na mgogoro wa kiuchumi unaoongezeka kwa kasi na kuibua hofu ya ongezeko jipya la wakimbizi kutoka Afghanistan.

Akizungumza wakati wa mkutano maalum wa kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya wahamiaji ya Umoja wa Mataifa naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa kundi hilo, Sher Mohammad Abbas Stanikzai, amesema ni jukumu la nchi kama Marekani, ambayo imezuia mabilioni ya dola, ili kuisaidia Afghanistan kujiimarisha upya baada ya miongo kadhaa ya vita. 

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Idhaa ya kiswahili (DW) Marekani imetoa mwongozo ambao unaweza kuruhusu pesa za kibinafsi kutumwa Afghanistan lakini haijabadilisha msimamo wake wa kuzuia dola bilioni 9 katika benki kuu au kuondoa vikwazo kwa baadhi ya viongozi wa Taliban. 

Waziri wa mambo ya ndani wa Taliban Amir Khan Muttaki amesema Taliban inakaribisha mashirika ya misaada ya kibinadamu na kuwahakikishia kwamba wataruhusiwa kufanya kazi bila vikwazo.

Waziri Mkuu Mstaafu atoa ushauri kwa machifu
Serikali kuja na mkakati huu sekta ya Afya