Waziri Mkuu Mstaafu,  John Malecela amewataka Machifu wote nchini kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan kuitawala nchi na kuendeleza amani iliyopo kwasababu bila amani hakuna kinachoweza kufanyika.

Malecela  ambaye ni mlezi  wa Umoja wa Machifu Tanzania (UMT), alitoa kauli hiyo jana  alipokuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa tisa wa UMT uliofanyika katika ukumbi wa Kibo Hotel Marangu  mkoani Kilimanjaro.

Amesema bila amani hakuwezi kuwa na maendeleo, bila amani hakuwezi kuwa na kuabudu kwa uhuru. “Kama nyumba  haina amani  hiyo inakuwa sio nyumba, nchi kama haina amani sio nchi hivyo ninyi Machifu mkamsaidie Rais (Samia Suluhu Hassan) wetu kuitawala nchi.” amesema Malecela

“Nianze kwa kuwahikikishia mimi nimekubali kuwa mlezi wa UMT nikiamini kwamba mimi na ninyi Machifu wote mlioko hapa tupo pamoja kuunga mkono serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.”

Serikali kuzindua kampeni ya kukabiliana na Uviko- 19
Viongozi wa Talibani waomba msaada