Beki na Nahodha wa Liverpool, Virgil van Dijk, amesema anaelewa wasiwasi wa watu kuhusu klabu hiyo kushindwa kufanya usajili wa nguvu kabla ya msimu mpya na amewataka wachezaji wenzake kuongeza kasi baada ya kuondokewa na wachezaji kadhaa muhimu.
Van Dijk mwenye umri wa miaka 32 alichukua nafasi ya Jordan Henderson kama nahodha baada ya kiungo huyo wa kati wa England kumaliza kuhudumu kwa miaka 12 Liverpool na kujiunga na klabu ya Saudi Pro League ya Al Ettihad mwezi uliopita.
Liverpool imepoteza wachezaji sita, huku Henderson na Fabinho wakihamia Saudi Arabia na viungo wenzake, Alex Oxlade-Chamberlain, James Milner, Naby Keita na mshambuliaji, Roberto Firmino wakiondoka kwa uhamisho huru.
Ikiwa msimu mpya unaanza kesho Ijumaa (Agosti 11), idadi ya waliowasili Anfield siyo ya kuridhisha, huku kiungo, Alexis Mac Allister na Dominik Szoboszlai wakíwa ndio wachezaji wawili pekee ambao Liverpool wamewasajíli katika mnsimu huu.
“Ninaweza kuelewa kwa njia fulaní,” alisema Van Dijk alisema alipoalizwa kuhusu wasiwasi wa mashabiki wa Líverpool.
“Ni wazi, wakati wachezaji wengi wanaondoka, nahodha wako anapoondoka, makamu wako anaondoka, naweza kuelewa baadhi ya watu wana mashaka.”
“Wacha tuangalie ikiwa wachezaji wengi wanaingia na tunapaswa kuwa tayari tena kwa msimu mrefu. Itakuwa ngumu sana tukiangalia timu zinazotuzunguka, lakini tunataka kuwa juu tena, tunataka kuwa na changamoto tena,” alisema Van Dijk.
“Lazima tujíamini. Tunapaswa kujiamini, na bado tunapaswa kujifunza kila siku.
“Kumekuwa na wahusika wanaoondoka, wachezaji ambao wamekuwa na mchango mkubwa katika mafanikio, lakini wengine wanapaswa kujitokeza. Hiyo changamoto nzuri kwa maoni yangu. Tunapaswa kufurahi.
Liverpool wataanza kampeni ya kuwania Taji la Ligi Kuu England kwa kufunga safari ya kuwafuata Chelsea, mechi itakayochezwa Jumapili (Agosti 13).