Beki na Nahodha wa Liverpool Virgil van Dijk anaweza kukumbana na adhabu zaidi kutoka Chama cha Soka England (FA) baada ya kuonekana kumtolea maneno makali mwamuzi aliyemwonyesha kadi nyekundu.

Van Dijk alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kipindi cha kwanza, wakati Liverpool ilipotoka nyuma na kuibuka na ushindi wa mabao 2-l dhidi ya Newcastle Utd.

Darwin Nunez alifunga mara mbili akitokea benchi na kuisaidia timu yake iliyokuwa na wachezaji 10 uwanjani kuibuka na ushindi ugenini.

Van Dijk anaweza kufungiwa kwa mchezo mmoja zaldi kutoka FA kwa kumnyooshea kidole mwamuzi John Brooks usoni, akionekana pia kutoa lugha isiyofaa. Van Dijk pia alibishana na mwamuzi wa akiba Cralg Pawson.

Kocha Yanga aipa ubingwa JKT
Robertinho aomba mechi za kirafiki