Mshambuliaji kutoka nchini Ujerumani Lukas Podolski atahamia nchini Japan mwishoni mwa msimu huu, baada ya kumalizana na klabu ya Galatasaray ya nchini Uturuki mwishoni mwa msimu huu.
Podolski ameitaja klabu ya Vissel Kobe ya nchini Japan ambayo atajiunga nayo kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31 ambaye aliwahi kuwatumikia mabingwa wa soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich amesema ni faraja kwake kuendelea na mipango ya kucheza soka katika bara lingine, tofauti na Ulaya alipopazoea.
Kabla ya kuthibitisha taarifa za kuelekea Japan mwishoni mwa msimu huu, Podilski alikua anahusishwa na mipango ya kuwaniwa na baadhi ya klabu za nchini China.
Msimu wa ligi ya nchini Japan ulianza mwishoni mwa juma lililopita, na Podolski atajiunga na klabu ya Vissel Kobe ikiwa tayari imeshacheza michezo kadhaa.
Mbali na FC Bayern Munich, Podolski aliwahi kucheza katika klabu za FC Köln, Arsenal na Inter Milan.