Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amemtaka Mbunge wa kuteuliwa, Humphrey Polepole kuwataja watu aliowaita ni wahuni aliosema hawakushughulikiwa wakati wa utawala wa Awamu ya Tano.
Kauli ya Nape imekuja kufuatia mahojiano yaliyofanywa kati ya Polepole na kituo cha televisheni cha Wasafi ambapo pamoja na mambo mengine, alisema udhaifu wa Serikali ya Awamu ya Tano ni kushindwa kuwamaliza wahuni.
“Mimi nilitamani sana kwenye uongozi wa Miaka Mitano ya Rais Magufuli tuwe tumeshughulika na watu wahuni wote na kuwamaliza, ukiniuliza udhaifu nitakwambia hatukuwamaliza wahuni, tungesgughulika na wahuni ulalo ulalo na kuwamaliza” alisema Polepole katika mahojiano hayo.
Akitoa maoni katika ukurasa wake wa Twitter, Nape amehoji kutokua na ufahamu kama kulikuwa na orodha ya wahuni wanaoshughulikiwa.
“Duh! Kumbe kulikuwa na orodha! Natamani kujua wahuni waliopona!
Nape Nnauye pamona na Humphrey Polepole wote wamewahi kuhudumu katika kiti cha Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi ambapi kwa hivi sasa kiti hicho kinakaliwa na Shaka Hamdu Shaka.