Jeshi la Polisi Zanzibar limesema kuwa limelazimika kufunga vituo vidogo katika Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja kutokana kukabiliwa na upungufu wa Askari visiwani hapo.

Hayo yamesemwa na Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame, amesema kuwa vituo hivyo vimefungwa na sasa vitalazimika kutumiwa na askari Jamii katika kuimarisha ulinzi.

“Tuna askari wachache ndiyo maana vituo vidogo tumelazimika kuvifunga na badala yake vitatumiwa na askari Jamii kutoa huduma za ulinzi katika maeneo yao.” amesema Kamishna Hamdan.

Aidha, amesema baada ya vituo hivyo kufungwa, wananchi wanatakiwa kuripoti matatizo yao katika vituo vya polisi vya karibu yakiwamo makosa ya uhalifu yanayotokea katika maeneo yao

Hata hiyo, amevitaja vilivyofungwa kuwa ni Vituo  vilijengwa chini ya mpango wa Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani, Augustino Mrema, ukiwa mkakati wake wa kupambana na uhalifu Zanzibar na Tanzania Bara.

 

Marekani yaionya Korea Kaskazini, 'Hatutakuwa na uvumilivu zaidi'
Video: Utekaji watikisa mahubiri Pasaka, Vituo vya Polisi vyafungwa kisa uhaba wa Askari Z'bar