Mshauri wa Rais Donald Trump wa masuala ya usalama, Herbert Raymond McMaster amesema kuwa Marekani na China zinaelekea kupoteza uvumilivu dhidi ya Korea Kaskazini inayoendelea na vitisho vya silaha za Nyuklia.

McMaster amesema makubaliano yanayojitokeza dhidi ya tabia ya vitisho ya Korea Kaskazini kwa sasa yanaijumuisha China. Amesema kuwa kuna makubaliano ya kimataifa, ikiwemo China kuhakikisha tabia hii haiendelei, kwani kumekuwa na majaribio ya makombora ya hivi karibuni yanayoonyesha tabia ya vitisho ya Korea Kaskazini hali ambayo hawataivumilia zaidi.

Amesema kuwa Rais Trump ameweka wazi kuwa Marekani na washirika wake hawatokubali kuona utawala wa vitisho dhidi ya silaha za nyuklia.

Korea Kaskazini imefanya jaribio la uzinduzi wa makombora ya masafa ya mbali, hata hivyo lilikwama, ambapo Makamu wa Rais wa Marekani, Mike Pence amefika nchini humo saa chache baada ya jaribio hilo.

Akizungumza katika kambi ya jeshi, Pence amesema anawahakikishia kuwa chini ya uongozi wa Rais Trump azimio la Marekani chini ya Korea Kusini, haujawahi kuwa na nguvu lakini kwa msaada Jeshi hilo na Mungu uhuru utaendelea kuimarika.

Video: Marekani yasema haitakuwa na subira tena dhidi ya Korea Kaskazini
Vituo vya Polisi Zanzibar vyapigwa kufuli