Matokeo ya kwanza ya uchaguzi wa bunge la Ulaya uliofanyika kwa siku nne yamethibitisha kuwa kambi ya vyama vikubwa vya siasa za wastani imepata pigo, huku uungwaji mkono wa kambi za Waliberali na walinzi wa mazingira ukiongezeka.

Kambi ya vyama vya Kihafidhina EPP imepata jumla ya viti 180 huku kundi la vyama vya Kisoshalisti na Democrats likipata viti 152.

Kambi ya Waliberali ALDE imepata uungwaji mkono mkubwa na kujinyakulia viti 105. Vyama vya walinzi wa mazingira vilikuwa katika nafasi ya nne na viti 67.

Aidha, nchini Ujerumani muungano tawala wa vyama vya siasa za wastani za mirengo ya kulia na kushoto vimeshuhudia uungwaji wake mkono ukiporomoka vibaya huku chama cha Kijani kinachotetea mazingira kikiibuka katika nafasi ya pili.

Uchaguzi wa rais wa Tume ya Ulaya na nyadhifa nyingine, utatokana na majadiliano baada ya nchi wanachama kuwasilisha uteuzi wao na bunge kuidhinisha wagombea wa mwisho katika miezi inayokuja.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya watakutana kesho Jumanne kuanza mchakato huo mgumu.

 

Kim Jong Un ampiga kijembe Trump, 'Huyu hajielewi na ana ufahamu mdogo'
Video: Homa ya ini tishio, Dar es salaam kupangwa upya