Mbunge Nusrat Hanje ambaye ni mleta maombi namba 15 katika kesi iliyofunguliwa na wabunge 19 wa viti maalumu (CHADEMA) wakipinga kufukuzwa ndani ya chama hicho, amedai kuwa vyama vya siasa vinauwa ndoto za vijana wengi, huku akikishangaa chama Chake (CHADEMA) kukana hakijamdhamini ili tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini (NEC), imteue kuwa mbunge viti maalumu.

Hanje, ametoa madai hayo hayo hii leo ijumaa (Novemba 4, 2022), mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu Masijala Kuu, Cyprian Mkeha wakati akihojiwa na wakili wa wajibu maombi Peter Kibatala ambaye alimhoji Nusrat kwamba, Chadema kupitia kiapo chake kinzani katika kesi hiyo, kinasema hakijamdhamini kuwa mbunge viti maalum.

Nusrat Hanje.

Amesema, hata alipokuwa gerezani akikabiliwa na shauri la jinai, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika walishirikisha mchakato wa kumtoa ndani na kusema, “Mwenyekiti na Katibu Mkuu walikuja gerezani nimesaini wakasema you don’t have to worry.”

Akijibu swali la Kibatala, la kwa nini katika madai yake hakuona ni suala la msingi kuiomba mahakama kuamua madai ya chama hicho kwamba hakijawahi kumteua kuwa Mbunge wa viti maalum sababu alikuwa gerezani, Nusrat amesema, “kuna mambo mengi ya kuyaongelea ndiyo maana nimekuja mahakamani.”

Wadaiwa sugu ardhi hatarini kupoteza umiliki
Akpan, Ouattara kupewa muda Simba SC