Marubani wa shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways, wataanza mgomo kesho Jumamosi (Novemba 5, 2022), kutilia mkazo madai yao ya mazingira bora ya kazi, licha ya mahakama ya nchi hiyo kuamuru mgomo huo usitishwe.

Kenya Airways, inayomilikiwa na serikali ya Kenya na shirika la ndege la Uholanzi KLM, ni mojawapo ya mashirika makubwa ya usafiri wa anga barani Afrika, ikiunganisha miji mingi katika mabara ya Afrika, Asia na Ulaya.

Marubani wa Ndege wakiwa kazini. Picha ya Kenya Invest.

Katibu Mkuu wa chama cha marubani wa Kenya Airlines, Kapteni Murithi Nyaga amesema hakuna ndege ya shirika hilo itakayopaa kutoka uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi kuanzia saa 12 asubuhi kesho Jumamosi.

Hata hivyo, amesema uongozi wa shirika hilo umeshindwa kushughulikia malalamiko ya marubani ambapo Kenya Airways nayo ilionya siku ya Jumatano (Novemba 2, 2022), kwamba malalamiko ya marubani hao hayana uzito wa kuhalalisha mgomo.

Kocha Mgunda aiwinda Singida Big Stars kiaina
Young Africans yachorewa ramani yote