Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Felix Tshisekedi amewataka Vijana wa nchi hiyo kuunda vikundi vya hadhari na kujiandikisha jeshini, ili kuwakabili waasi wa M23 waliopo mashariki mwa nchi hiyo.

Rais Tshisekedi, ametoa wito huo katika hotuba yake aliyoitoa kwa njia ya televisheni, huku akiwashutumu waasi wa M23 kuwa na usaidizi wa kijeshi toka nchini Rwanda, akisema inataka kujitanua kieneo.

Amesema, Rwanda ina malengo ya kupora madini ya Kongo kwa kuyumbisha usalama wa eneo la mashariki ili kukidhi alichokiita ”hamu yake ya kihalifu.”

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Felix Tshisekedi. Picha ya Michele Tantussi/ Getty Images

Rais Tshisekedi pia amesema, juhudi za kidemokrasia zimeshindwa kuzaa matunda na kuongeza kuwa mzozo wa sasa unahitaji kujitolea kwa raia wote wa Kongo.

Hata hivyo, Tshisekedi ameonya unyanyapaa wa raia wa nchi hiyo wanaozungumza lugha ya Kinyarwanda ambapo mara zote Rwanda imekanusha kuwasaidia waasi wa M23, na kusema wanayo madai ya msingi.

Maandalizi urejeshaji madhari ya Misitu yakamilika
Ukraine yalia na Urusi uharibifu miundombinu ya nishati