Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amesema mashambulizi ya Urusi dhidi ya miundombinu ya nishati imewaacha takriban watu milioni 4.5 bila umeme.

Kwa wiki kadhaa sasa, vikosi vya Urusi vimerusha makombora na kuongeza mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani kulenga vituo vya Ukraine na kuharibu theluthi moja ya mitambo ya nishati.

Waokoaji wa Ukraine wakizima moto baada ya roketi kugonga kifaa cha miundombinu ya umeme huko Kharkiv, wakati uvamizi wa kijeshi wa Urusi. Picha: EPA-EFE/SERGEY KOZLOV

Aidha, katika kile kinachoaminika kuwa malengo ya kuvunja ari ya raia wa Ukraine na mataifa jirani wakati huu wa msimu wa baridi, shambulio hilo limeonekana kuiathiri Ukraine.

Hapo jana (Novemba 3, 2022), Mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la nchi saba zilizostawi kiviwanda, G7 walikutana kujadili namna watakavyoratibu msaada zaidi kwa Ukraine kufuatia mashambulizi yanayofanywa na Urusi dhidi ya mifumo ya nishati yalisosababisha ukosefu wa huduma ya umeme.

Rais awahimiza vijana kujiandikisha Jeshini
Mhandisi Chiwelesa: TANROADS isipewe miradi ya ujenzi viwanja vya ndege