Serikali nchini, imesema imekamilisha maandalizi ya mkakati wa Kitaifa wa kurejesha mandhari ya Misitu wenye lengo la kuondoa ardhi iliyoharibika kutokana na shughuli za kibinadamu.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni jijini Dodoma, hii leo Novemba 4, 2022.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja.

Waziri Mary alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Donge, Mohamed Soud aliyetaka kujua kampeni ya AFR imetekelezwa kwa kiasi gani.

Serikali imekuwa ikihimiza idara zake kuhakikisha inasimamia ulinzi wa rasilimali za Taifa ikiwemo uangalizi wa vyanzo vya maji ambavyo vinaharibiwa na shughuli za kibinadamu.

Wauguzi watakiwa kutumia lugha za staha kwa Wagonjwa
Rais awahimiza vijana kujiandikisha Jeshini