Serikali ya nchi ya China, imeifutia Tanzania deni la shilingi billion 31.4 ambalo ilikuwa inaidai Tanzania na kusaini baadhi ya mikataba ya makubaliano, baina ya nchi hizo mbili.

Makubaliano hayo, ni uwepo wa soko la kusafirisha maparachichi toka nchini kwenda China, soko la mabondo ya samaki na vitu vingine vitokanavyo na samaki ambapo pia imeikopesha Tanzania Dola milioni 56.7 kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa ndege Zanzibar, terminal III.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Xi Jinping wakati akikagua Gwaride la Heshima katika ukumbi wa The People Great Hall, Beijing nchini China tarehe 03, Novemba, 2022.

Hersi Said: Wapuuzeni wasioitakia mema Young Africans
Tafiti: Watanzania wengi wanaishi na kisukari