Jumla ya Mawakili mashuhuri 40 wa nchini Iran wanaotetea haki za binaadamu, wamewakosoa hadharani viongozi wa kidini wakisema utawala uliopo utaondolewa madarakani, kufuatia waandamanaji kote nchini humo kutoogopa tena kamata kamata inayofanywa na serikali dhidi yao.

Mawakili hao, ambao baadhi yao ni wa kutoka ndani ya nchi na wengine nje ya nchi wamesema serikali ya Iran inaendelea kuota na ikiamini inaweza kukandamiza, kukamata na kuua kwa lengo la kunyamazisha umma kitu ambacho ni kinyume.

Rais wa Iran, Ebrahim Raisi. Picha: AP

Maandamano nchini humo, yamechochewa na kifo cha msichana Mahsa Amini (22), kilichotokea wakati alipokamatwa na Polisi wa maadili, kufuatia kutovalia vizuri hijabu yake na kuhusishwa na uvunjifu wa sheria za dini ya kiislamu.

Hata hivyo, maandamano hayo yameliyumbisha tabaka la mashehe, huku kiongozi Mkuu Iran, Ayatollah Ali Khamenei na Rais wa taifa hilo, Ebrahim Raisi wakiungana na viongozi wa kidini na watu wa matabaka mbalimbali nchini humo, kudai mabadiliko ya kisiasa katika Jamhuri hiyo ya kiislamu.

Tafiti: Watanzania wengi wanaishi na kisukari
Njaa, Utapiamlo vyashika kasi maeneo yenye ukame