Idadi ya waliojitokeza katika duru ya pili ya uchaguzi wa bunge nchini Tunisia, asilimia 11.3 huku vyama vya upinzani vikisusia uchaguzi huo kwa kile kinachoonekana kukataa wazi mageuzi yenye utata ya Rais Kais Saied.
Uchaguzi huo, ulionekana kuwa mtihani baada ya Rais Saied kujiimarisha lakini uhalali huo sasa unatiliwa shaka kutokana na idadi ndogo ya waliojitokeza kupiga kura tofauti na duru ya kwanza iliyofanyika Desemba 2022.
Bunge la mwisho, likiongozwa na Chama cha Kiislam cha Ennahdha, lilisimamishwa 2021 na baadaye kuvunjwa na Saied ambapo pia alibadilisha katiba ya nchi ili kupunguza mamlaka ya bunge, na kujipa uhuru zaidi.
Saied alisema, ”Tunachojua kuhusu uchaguzi Katika duru ya kwanza, wagombea 10 walipata viti bila kupata kura zozote, kwani walijitokeza bila kupingwa. Kwa majimbo saba, hakukuwa na wagombea. Maafisa wa uchaguzi walisema viti hivyo vitajazwa katika uchaguzi maalum baadaye”.
Mashirika huru kama vile Chahed (Shahidi), na Mourakiboun (Wadhibiti), walisema baadhi ya wakuu wa vituo vya kupigia kura walikataa kuwapa waangalizi upatikanaji wa data juu ya watu waliojitokeza kupiga kura.
Makamu wa rais wa Umoja wa Kitaifa, na Waandishi wa Habari wa Tunisia, Amira Mohamed, alisema kwenye Redio ya Mosaique kwamba waandishi wa habari walizuiwa kutoka katika baadhi ya vituo vya kupigia kura.
“Bunge lijalo halina mamlaka juu ya serikali. Kwa hiyo kwa wabunge wanaotoa ahadi kwa wananchi, watatekeleza ahadi zao kwa utaratibu gani?” mkuu wa chama Abdellatif Meki aliambia shirika la habari la Associated Press.
Baadhi ya wananchi wa Tunisia awali walikaribisha unyakuzi wa Saied wa mamlaka mwaka 2021, baada ya serikali za awali kushindwa kufufua uchumi au kuboresha huduma za umma.