Aliyekuwa mpinzani wa Mwenyekiti wa Simba SC Murtaza Mangungu kwenye Uchaguzi Mkuu wa Klabu hiyo Moses Kaluwa amesema, ataendelea kutoa ushirikiano kwa viongozi wenzake licha ya kushindwa.

Kaluwa amezungumza hayo baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Boniface Lihamwike kutangaza matokeo ya Uchaguzi uliofanyika Ukumbi wa Kimataifa Julius Nyerere ‘JNICC’ jijini Dar es salaam.

“Nichukue nafasi hii kuwashukuru kwa wale wote walionipa kura zao, Simba SC ni kubwa kuliko mtu yeyote hivyo niseme wazi kwamba nitashirikiana na viongozi wote waliokuwa madarakani.”

Katika uchaguzi huo ambao matokeo yake yametangazwa leo Jumatatu (Januari 30) Afajiri, Kaluwa amepata kura 1,045 huku Mangungu ambaye alikuwa anatetea kiti chake akipata jumla ya kura 1,311.

Kwa upande wa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi walioshinda ni Dr Seif Ramadhan Muba (1636), Asha Baraka (1564), CPA Issa Masoud Iddi (1285), Rodney Chiduo (1267) na Seleman Harubu (1250).

Jumla ya Wanachama Simba SC waliopiga Kura ni 2363 Kura halali, lakini Kura halali zilikuwa 2356.

Aliyeteswa na ndoto za kichawi miaka 10 asimulia mazito
Vyama vya upinzani, wananchi wasusia uchaguzi