Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amewataka waajiri kuweka mikakati ya kuhakikisha inaondoa mambo yanayosababisha matatizo ya akili.
Ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya afya ya akili duniani, ambapo amesema kuwa ikiwa afya ya akili itakuwa sehemu ya ajenda mahali pa kazi, itawezesha matibabu ya mapema kwa walio na dalili za magonjwa hayo, hivyo kupatiwa tiba.
Amesema kuwa taarifa za afya na magonjwa ya akili ya mwaka 2015/16 inaonyesha takriban wagonjwa 611,789 wamehudhuria vituo vya kutolea huduma ya afya nchini ili kuweza kuondokana na tatizo hilo.
“Hii ni kwa sababu ndipo sehemu ambayo mwajiriwa na mwajiri wanakaa muda mrefu kuliko muda wa majumbani, hivyo ni vyema wakahakikisha masuala mazima ya vipimo yanafanyika,” amesema Ummy Mwalimu.
Aidha, amesema kuwa kufanya hivyo kutapunguza unyanyapaa, kutengwa na kunyanyaswa, hivyo kuifanya jamii kuongeza uelewa na kutambua magonjwa ya akili kama magonjwa mengine na hivyo kuyapa kipaumbele.
-
Ndugai awanong’oneza mawaziri wateule
-
Polisi watunukiwa tuzo na Wananchi
-
Video: LHRC chataka adhabu ya kifo ifutwe
Hata hivyo, ameongeza kuwa katika kukabiliana na wimbi la ugonjwa wa afya ya akili wataalamu na waajiri wataendelea kuelimisha jamii juu ya magonjwa ya akili na kupinga vitendo visivyofaa.