Mgomo mpya wa kupinga marekebisho ya umri wa kustaafu nchini Ufaransa, umeathiri mambo mbalimbali katika nchi hiyo, ikiwemo usafiri wa umma, wanafunzi kutokwenda shule na upatikanaji wa huduma ya umeme.
Maandamano hayo ambayo ameingia siku ya nne, pia yameathiri shughuli za ugavi wa mafuta na gesi na yamehudhuriwa na maelfu ya watu wanopinga marekebisho ya Serikali ya pensheni.
Aidha, upingaji huo wa marekebisho ya umri wa kustaafu, unafanyika ikiwa ni siku moja baada ya wabunge wa Ufaransa kuanza kujadili muswada huo.
Muswada huo wa pensheni, unalenga kuongeza umri wa chini wa kustaafu kutoka mika 62 hadi 64 na Rais Emmanuel Macron anaunga upitishwe kuwa sheria.