Polisi nchini Kenya, wametumia gesi ya kutoa machozi dhidi ya waandamanaji waliokusanyika nje ya jengo la bunge, wakipinga muswada wa fedha uliopendekezwa na ambao umezua utata.
Polisi walijaribu kuwatawanya karibu waandamanaji 500 waliokuwa wakiwasilisha malalamiko yao ya kupinga muswada huo bungeni ambapo unaolenga kuongeza kodi ya mafuta na makazi.
Rais wa nchi hiyo, William Ruto mwaka jana (2022), alitoa ahadi za kusaidia watu wa kipato cha chini, lakini sasa anaonekena kukabiliwa na shinikizo la kuongeza mapato ya serikali, ili kukabiliana na deni kubwa lililopo.
Hata hivyo, pendekezo lake la kuongeza ushuru linakosolewa vikali na wafanyakazi wa serikali pamoja na viongozi wa upinzani ambao wanasema kwamba gharama ya maisha tayari ipo juu zaidi.