Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit amepongeza hatua iliyofikiwa baina ya pande mbili hasimu baada ya maelfu ya waasi wa zamani wameapa kiapo cha uaminifu katika hafla iliyofanyika chini ya ulinzi mkali nchini humo.
Takriban wanaume na wanawake 22,000 kutoka vyama vikuu na vile vile Muungano wa Upinzani wa Sudan Kusini, walishiriki katika uapisho huo, shughuli ambayo ilipangwa kufanyika mwaka 2019 kwa mujibu wa makubaliano.
Katika uapisho huo, Rais Salva Kiir Mayardit amesema kati ya sura zote za makubaliano, kuhitimu kwa vikosi vilivyoungana chini ya sura ya pili kulikuwa changamoto kubwa na muhimu zaidi kutokana na watu 200 kufariki katika vituo 18 vya mafunzo,
Kwa upande wake, Makamu wa Rais na kiongozi wa upinzani, Riek Machar amesema, “Wengine walikufa kwa sababu ya ugonjwa na kukosekana kwa dawa, huku wengine wakifa kwa njaa kwani chakula hakikupatikana kwa wakati sahihi na kwa muda mrefu.”
Naye, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu na Mkuu wa UNMISS, Nicholas Haysom amesema kikosi cha ulinzi kilichounganishwa ni mojawapo ya matokeo yanayoonekana na yenye maana zaidi ya umoja wa kitaifa, hasa katika jamii zinazotokana na migogoro.