Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella amewataka wananchi wa mkoa huo kujenga uzalendo kwa kufanya kazi na kulinda rasilimali za nchi ili ziweze kuwanufaisha wao, vizazi vya sasa na vijavyo.
Amesema kuwa ulinzi wa rasilimali za nchi ni mhimu ili ziweze kunufaisha jamii kwa ujumla, hivyo ni vyema wakajijengea tabia ya kuhoji.
“Tujiulize, mimi ni mzalendo kwa jamii na taifa langu? Kufanya kazi ni uzalendo wa kutosha na unaongeza tija katika kuboresha uwezo, kuitikia na kushiriki shughuli za kijamii na hivyo kila mmoja awajibike kwa kujenga uzalendo kwa mkoa wetu na taifa letu,”amesema Mongella.
Aidha, ameikumbusha jamii kupanda miti ili kutunza na kulinda mazingira na kuacha kukata miti hiyo ovyo, kuchimba mchanga, kupasua mawe ili kuweza kuondokana na uharibifu.
Kwa upande wake Afisa Mazingira wa Asasi isiyo ya kiserikali (TECO), John Masweta ameshauri kuwe na utaratibu wa
kupanda misiti mikubwa.
-
LHRC champongeza JPM
-
Madereva 43 waanza kupatiwa mafunzo ya huduma ya kwanza
-
Wizara ya Fedha na Mipango yashinda tuzo
Hata hivyo, Mkuu wa Kikosi cha Anga 601 KJ Meja Bryceson Msilu amesema kuwa ili kukabiliana na uharibifu wa mazingira kwa kushirikiana na TECO wamepanda jumla ya miti 3,400 kuanzia Disemba mosi mwaka huu na wanatarajia kupanda miti 3,000 ya matunda katika maeneo mbalimbali ya taasisi za umma jijini Mwanza