Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli kufuatia kuuawa kwa askari wake 15 waliokuwa wakilinda amani nchini Kongo.

Katika barua hiyo, Rais Kenyatta amesema kushambuliwa kwa askari ambao walikuwa wakitoa huduma ya kulinda amani nchini Kongo haikubaliki.

Aidha, amesema kuwa Kenya itaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kulinda amani ya Kongo na maeneo ya maziwa makuu,

Hata hivyo, Mwishoni mwa wiki iliyopita askari 15 wa JWTZ waliokuwa wakilinda amani nchini Kongo walishambuliwa na waasi wanaoendesha mpigano nchini humo, hivyo kupelekea vifo.

Waaswa kulinda rasilimali za taifa
Msuva: Sitamani tupangwe dhidi ya Yanga