Baraza Kuu la Uongozi la Chama cha Wananchi (CUF) Linalomuunga Mkono Prof. Ibrahim Lipumba limewavua uanachama Wabunge 8 wa Viti Maalum na Madiwani 2 wa chama hicho kwa kosa la kukisaliti chama.
Wabunge hao 10 na madiwani wawili wa CUF, wanaomuunga mkono, Katibu Mkuu, Seif Shariff Hamad jana waliiitwa kwa ajili ya mahojiano katika Ofisi za Chama cha Wananchi (CUF) lakini walikaidi wito huo wa kutokuonekana katika ofisi hizo.
Aidha, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama cha Wananchi (CUF) limewavua uanachama wabunge wanane wa chama hicho kwa madai ya utovu wa nidhamu, yakiwemo kukisaliti chama hicho.
Mwenyekiti wa CUF, anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba amesema, baraza pia limewavua uanachama madiwani wawili wa viti maalumu mkoani Dar es Salaam, kwa makosa kama hayo.
-
Mbunge wa Jimbo la Temeke aswekwa rupango
-
Msigwa amkosoa vikali Ndugai, naye ajibu mapigo
-
Polisi: Lissu hatoki Ng’o, mpaka upelelezi ukamilike
“Leo asubuhi tumewasilisha nyaraka za hatua hizi kwa Spika na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa hatua zaidi,” amesema Profesa Lipumba.
Amesema wabunge hao wanane ni kati ya 10 walioitwa hivi karibuni na Kamati ya Maadili na Nidhamu kwa mahojiano wakitakiwa kujibu tuhuma zinazowakabili za kukihujumu chama hicho kwa maelezo kuwa walitaka kushirikiana na Chadema kumwondoa yeye madarakani