Bunge la Pakistan limepiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu Imran Khan siku ya Jumapili, huku wabunge 176 kati ya 342 wakipiga kura dhidi yake.

Spika wa bunge Asad Qaisar, ambaye pia ni mwanachama wa chama cha Khan, alitangaza kujiuzulu baada ya kuahirisha bunge mara tatu siku ya Jumamosi.

Chama cha Khan PTI kilipoteza idadi ya wabunge katika Bunge hilo mwezi Machi baada ya wabunge saba wa chama shirika kuamua kujiunga na safu ya upinzani.

Wapinzani hao walimtuhumu nyota huyo wa kriketi aliyegeuka kuwa mwanasiasa kwa kushindwa kusimamia uchumi wa Pakistan, ulioathiriwa na janga la UVIKO-19, na pia kushughulikia sera ya kigeni na ya ndani ya Islamabad.

Hoja ya Jumapili ina maana kwamba muhula wa miaka mitano wa Khan umemalizika mapema, sawa na ule wa mawaziri wakuu wote waliopita wa nchi hiyo.

Kocha Orlando Pirates aihofia Simba SC Kwa Mkapa
CBF yamtengea Pep Guardiola Pauni Milioni 10