Wachezaji wa klabu ya Arsenal, wamekubali kukatwa asilimia 12.5 ya mishahara yao, baada ya kuahidiwa ‘bonasi’ kubwa katika ligi ya mabingwa Ulaya.
Wachezaji watafidia fedha watakazokatwa kwa kila mmoja kulipwa pauni laki moja (£100,000), endapo watafuzu kucheza msimu ujao wa ligi ya mabingwa ya Ulaya.
Klabu pia, imeahidi kumlipa kila mchezaji bonasi ya pauni laki tano (£500,000) kama watatwaa taji la ligi ya mabingwa Ulaya mwaka 2021 au pauni laki moja (£100,000) kama wataibuka mabingwa wa ligi ya Europa.
Arsenal, imekuwa klabu ya kwanza ya ligi kuu England, kukubali mpango wa kukata mishahara kwa wachezaji wake, katika kipindi hiki ambacho klabu nyingi duniani zimeathirika kiuchumi kutokana na janga la virusi vya Corona.