Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Henry Mayala akimpima mchezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Simba kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi wakati wachezaji wa timu hiyo walipofika JKCI kwaajili ya kupima vipimo mbalimbali vya moyo na damu. Timu hiyo inatarajia kushiriki mashindano ya kimataifa na wachezaji wake wanafanya vipimo hivyo ikiwa ni mojawapo ya kutekeleza sheria ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa kila mchezaji anayeshiriki mashindano hayo kupima.
Fundi sanifu wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Gerson Mpondo akiwaelezea wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Simba namna kipimo cha kuangalia mfumo wa umeme wa moyo kinavyofanyika wakati wachezaji hao walipofika JKCI kwa ajili ya kupima vipimo mbalimbali vya moyo na damu. Timu hiyo inatarajia kushiriki mashindano ya kimataifa na wachezaji wake wanafanya vipimo hivyo ikiwa ni mojawapo ya kutekeleza sheria ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa kila mchezaji anayeshiriki mashindano hayo kupima.
Mfanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Lusina Salum akichukua taarifa za mchezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Simba Inonga Hemock wakati wachezaji wa timu hiyo walipofika JKCI kwaajili ya kupima vipimo mbalimbali vya moyo na damu. Timu hiyo inatarajia kushiriki mashindano ya kimataifa na wachezaji wake wanafanya vipimo hivyo ikiwa ni mojawapo ya kutekeleza sheria ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa kila mchezaji anayeshiriki mashindano hayo kupima.
Mteknolojia wa mionzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Abdala Kaniki akiwapa maelezo wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Yanga namna kipimo cha X-ray ya kifua kinavyofanyika kwa ajili ya kuangalia kama mapafu na moyo yako sawa wakati wachezaji hao walipofika JKCI kwa ajili ya kupima vipimo mbalimbali vya moyo na damu. Timu hiyo inatarajia kushiriki mashindano ya kimataifa na wachezaji wake wanafanya vipimo hivyo ikiwa ni mojawapo ya kutekeleza sheria ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa kila mchezaji anayeshiriki mashindano hayo kupima.
Mteknolojia wa mionzi Abdala Kaniki kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) akimpima mchezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Yanga Gael Bigirimana kipimo cha X-ray ya kifua kwaajili ya kuangalia kama mapafu na moyo yako sawa wakati wachezaji hao walipofika JKCI kwaajili ya kupima vipimo mbalimbali vya moyo na damu. Timu hiyo inatarajia kushiriki mashindano ya kimataifa na wachezaji wake wanafanya vipimo hivyo ikiwa ni mojawapo ya kutekeleza sheria ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa kila mchezaji anayeshiriki mashindano hayo kupima.
Mteknolojia wa mionzi Abdala Kaniki kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) akimpima mchezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Yanga Joyce Lomalisa kipimo cha X-ray ya kifua kwaajili ya kuangalia kama mapafu na moyo yako sawa wakati wachezaji hao walipofika JKCI kwaajili ya kupima vipimo mbalimbali vya moyo na damu. Timu hiyo inatarajia kushiriki mashindano ya kimataifa na wachezaji wake wanafanya vipimo hivyo ikiwa ni mojawapo ya kutekeleza sheria ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa kila mchezaji anayeshiriki mashindano hayo kupima.